Daktari apachika kamera vyooni

Image caption Daktari aweka kamera za siri Chooni

Daktari mmoja aamua kufanya kile ambacho hakikutegemewa na wengi, kwa kupachika kamera kwa siri katika vyoo vilivyoko katika hospitali anayofanyia kazi na kufanikiwa kuwa chungulia wagonjwa wapatao 100 walipokuwa wakijisaidia na idadi hiyo ni watu wazima na watoto.

Dokta Lam Hoe Yeoh almaarufu Robin mwenye umri wa miaka 61 anayetokea BansteadSurrey,anatuhumiwa kwa makosa 30 yakiwemo makosa mawili ya kuchungulia watoto na kuwarekodi,na makubwa Zaidi ni yanayo karibia kua ya kingono.

Image caption Daktari aweka kamera za siri Chooni na kuwatizama zaidi ya watu 100

Inaelezwa kwamba alikamatwa mapema mwaka huu akiwa katika hospitali binafsi ya St Anthony iliyoko kaskazini . Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo ameiahirisha mpaka September 16 mwaka huu wakati ambapo dokta Yeoh atakapoyakabili mashtaka,na yaelezwa dokta huyo anashikiliwa lupango.