Wanajeshi wa Nigeria warejea nyumbani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Majeshi 480 wa Nigeria watorokea Cameroon

Wanajeshi 480 wa Nigeria waliokuwa wametorokea maisha yao nchi jirani ya Cameroon kufuatia makabiliano makali dhidi ya wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram wamerejea makwao.

Msemaji wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali Didier Badjek amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wanajeshi hao waliokuwa wamepokonywa wamerejea nchini Nigeria..

Mapigano bado yanaendelea karibu na mji ulioko mpakani wa Gamboru Ngala.

Mapigano hayo yanawadia saa chache tu baada ya wapiganaji hao wa Boko Haram kutoa kanda ya video ambayo walitangaza kuundwa kwa himaya ya Kiislamu kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi hao walikuwa wakikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.

Haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii Muungano wa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.

Msemaji wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade alipinga tangazo hilo akisema kuwa ''hakuna hata nchi moja ya taifa hilo iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni moja. ''

Haki miliki ya picha n
Image caption Kiongozi wa Boko Haram Shekao ametangaza himya ya KIislamu Kaskazini mashariki mwa Nigeria

Maelfu ya watu wameuwawa kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu 2009, wakati Boko Haram ilipoanza uasi wake.

Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.

Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema.