Pooley atajwa kuwa shujaa wa Ebola

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wiliam Pooley

William Pooley anayetibiwa mjini London, baada ya kupata maambukizo ya Ebola, anatunzwa vizuri

Familia ya muuguzi huyo wa kujitolea, aliyesafirishwa mjini London, baada ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, wamesema amekuwa akipata matunzo yaliyo bora.

Willliam Pooley mwenye umri wa miaka 29 alirudi nchini Uingereza siku ya Jumapili na amewekwa kwenye kitengo maalumu katika hospitali ya Royal Free.

Bwana Pooley ambaye alikuwa amejitolea kuwahudumia wagonjwa wa mlipuko wa Ebola barani Afrika ambao umeuwa watu 1,500 ametajwa kama shujaa na taasisi moja ya hisani inayojulikana kama Shepherd Hospice aliyoifanyia kazi nchini Sierra Leone kwa vile alijua hatari zilizokuwepo lakini akaamua kusaidia.

Bwana Pooley anayetoka karibu na mji wa Woodbridge, katika kaunti ya Suffolk ni Mwingireza wa kwanza kupatikana na virusi vya Ebola katika mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea hivi karibuni.