Msumbiji:Serikali na Renamo waafikiana

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Renamo nchini Msumbiji

Habari kutoka Msumbiji zinasema serikali ya nchi hiyo imetiliana saini na chama cha upinzani cha Renamo ili kumaliza uhasama kuelekea uchaguzi wa mwezi Oktoba.

Mkataba huo unafuatia unafuatia mapigano ya chini kwa chini kati ya wafuasi wa Renamo wenye silaha na majeshi ya serikali. Mwezi Oktoba mwaka jana Renamo walijitoa katika mkataba wa amani uliotiwa saini kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita, mkataba ambao ulimaliza vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe. Wiki iliyopita ikiwa sehemu ya makubaliano, serikali ya Msumbiji ilianza kuwaachilia wafungwa wa Renamo waliokuwa wamekamatwa katika mapigano ya hivi karibuni.

Tangu Msumbiji ijipatie uhuru wake tarehe 25 Juni 1975 kutoka kwa wakoloni wa Kireno imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na waliokuwa waasi wa renamo na sasa ni chama cha siasa cha upinzani.