IS ilikiuka haki za kibinadamu Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ripoti ya UN imesema kuwa IS ilikiuka haki za kibinadamu Syria

Umoja wa Mataifa umewashtumu , wanamgambo wa Islamic State kwa kuwahujumu watu mara kwa mara mbali na kuwasajili watoto kuhudumu kama wanajeshi.

Wakati huohu UN imeistuhumu serikali ya Syria kwa kutumia kemikali aina ya Chlorine katika matukio manane katika ripoti mpya kuhusu uhalifu wa vita nchini humo.

Islamic State ambayo kwa sasa inadhibiti sehemu kubwa ya Syria ni moja ya vikundi ambavyo vinapigana na serikali ya rais wa Syria ,Bashar al-Asaad.

Zaidi ya watu laki mbili wameuawa tangu vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe kutibuka mwaka wa 2011.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watoto walilazimishwa kujiunga na jeshi la IS

Ripoti hiyo ni kufuatia mahojiano ya miezi sita na ushahidi uliotafutwa kati ya mwezi wa January na Julai mwaka huu kama sehemu ya uchunguzi wa ukiukwaji kwa haki za binadamu ndani ya Syria.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba miili ya wale walio uawa huwa inawekwa kwa maonyesho kwa siku kadhaa kitu ambacho hutishia wakaazi wa huko.

Aidha wanawake wamepigwa kwa kutovalia hijabu huku wale wanaoshtumiwa kwa usherati wakipigwa mawe hadi kufa hadharani.

Mjini wa Raqqa, watoto wachanga wenye umri wa miaka 10 wanapewa mafunzo katika kambi za IS.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serikali ya Syria nayo ilitumia kemikali mara 8

Bwana Paulo Pinheiro, alionya kuwa kundi hilo IS litaathiri eneo zima la ghuba.''Jamii ya kimataifa ilifeli kutekeleza wajibu wake mkubwa wa kulinda maisha ya raiya dhidi ya ukiukwaji wa haki zao za kibinadamu ''.

Wachunguzi hao walionya kuwa vita hivyo vinakila dalili ya kuenea kwa mataifa yaliyoko karibu.

Mmoja wa wachunguzi hao wa kimataifa Carla del Ponte, ameoamba jamii ya kimataifa kuishatki Syria katika mahakama ya ICC kama vile ilivyofanya dhidi ya Rwanda.