Wanajeshi walivuka bahati mbaya:Urusi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption majeshi ya Urusi

Urusi imesema wanajeshi wake kumi wanaoshikiliwa nchini Ukrain walivuka mpaka kwa bahati mbaya.

Serikali ya nchi hiyo imesema kuwa wanajeshi hao walikuwa katika shughuli ya kawaida ya ukaguzi wa mipaka katika yake na Ukraine na ghafla wakajikuta wapo nchini humo na kasha wakakamatwa katika kijiji cha Dzerkalne .

Hata hivyo eneo hilo walilokamatwa askari hao wa Urusi ni zaidi ya kilomita 20 kutoka mpakani mwa Urusi na Ukraine.

Televisheni ya taifa la Ukraine imeonyesha picha zinaonyesha kuwa askari hao walidhamiria kuvuka mipaka.

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko anatarajiwa kukutana viongozi wa Urusi kwa majadiliano Zaidi.