Balozi wa Guinea amjeruhi mwanawe

Image caption Polisi wa jiji la Washington

Polisi nchini Marekani wameshindwa kumkamata balozi wa Equatorial Guine mjini Washngton, kwa tuhuma za kumpiga binti yake kwa mguu wa kiti cha mbao, balozi huyo hajakamatwa mpaka sasa kutokana na kinga yake ya kibalozi alonayo .

Msemaji wa polisi Dustin Sternbeck amesema kwamba walipewa taarifa mapema wiki hii kua kuna tukio nyumbani kwa balozi huyo, na walipofika wakamkuta binti huyo mdogo akiwa na jeraha kubwa kichwani mwake ambaye alihitaji tiba na hivyo kumpeleka hospitalini kwa matibabu.

Pamoja na hayo yote Dustin alisema kua polisi hawana mamlaka kwa kesi za namna hiyo zinazowahusisha wanadiplomasia lakini wamekwisha iarifu serikali juu ya suala hilo.