Panda adanganya ana mimba

Image caption Ai Hin akijilia mianzi kwa raha zake.

Ripoti kutoka nchini China zaeleza kwamba, Panda mmoja mkubwa jike aliamua kuwachezea shere wale wanaomhudumia kwa kuwaonesha kila dalili kua ana mimba ili apewe aina ya mikate ya buns zaidi.

Panda huyo aitwaye Ai Hin, alianza kuonesha dalili zote za mimba katika kituo cha utafiti na upandikizaji wanyama kilichoko katika jimbo la Sichuan,China.

Kutokana na kuonesha dalili hizo, mipango ikaanza kupangwa ya kuja kumzalisha panda Ai Hin kwenye runinga live watu washuhudie, naye panda huyo sijui alistukia mpango huo? Tabia na dalili za mimba zikatoweka na kuwa katika hali ya kawaida.

Mtaalamu wa wanyama alipoulizwa nini kimetokea, alisema kua pengine Panda huyo aling'amua kua Panda wazazi huondolewa kwenye vyumba vilivyopozwa hewa na kwenda kufungiwa sehemu chini ya uangalizi maalum na huko hupewa nyongeza ya matunda na buns nyingi na zaidi huongezewa mianzi mingi.

Kwa tabia Panda huzaa kwa nadra sana na wale wanaofungiwa robo yao huwa hawazai.