Nigeria yazindua vitambulisho vyake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfano wa kitambulisho cha Uraia Nigeria

Nchi ya Nigeria imezindua mpango wa vitambulisho vya taifa hilo vya ki- elektroniki .Raisi Goodluck Jonathan amekua mtu wa kwanza kupata kadi hiyo ya BIOMETRIC CARD, baada ya kuipokea ameielezea kadi hiyo kua itarahisisha huduma za Kiserikali lakini pia kadi hiyo inao uwezo wa kufanya malipo mtandaoni .

Baada ya uzinduzi huo,imebainika kwamba Wanaigeri wote watapaswa kua na kadi hiyo mpaka kufikia mwaka 2019 endapo watakua na haja ya kupiga kura.

Jaribio la kutaka taifa la Nigeria kua na vitambulisho vya taifa la Nigeria lilishindwa miaka kumi iliyopita kutokana na rushwa