Jeshi lazingira makao ya polisi Lesotho

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeshi la Lesotho

Ripoti kutoka Taifa la kusini mwa Afrika Lesotho zinasema kuwa jeshi limezingira makao makuu ya polisi na kuzuia matangazo ya radio pamoja na mtandao wa simu katika mji mkuu wa Maseru.

Shirika la habari la AFP limemnukuu waziri wa habari Thesele Maseribane akisema kuwa milio ya risasi ilisikika na kukilinganisha kisa hicho na jaribio la mapinduzi .

Uchaguzi ambao haukukamilika nchini humo miaka miwili iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti.

Licha ya mazungumzo ya kuleta amani mnamo mwezi Juni ,hali ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo wakionya dhidi ya mbinu yoyote isio ya kikatiba.

Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana jirani yake kwa mali asli pamoja na ajira.