Waziri mkuu wa Lesotho atorokea A.kusini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeshi la Lesotho

Waziri mkuu nchini Lesotho Tom Thabane ameiambia BBC kwamba amelitoroka taifa hilo baada ya kupata vitisho vya maisha yake.

Akizungumza kutoka nchini Afrika kusini,Bwana Thabane amesema kuwa vitenmdo vya jeshi nchini humo vimesitisha huduma za serikali na kusababisha mapinduzi.

Awali Ripoti kutoka mji mkuu wa maseru zilizsema kuwa jeshi lilizingira makao makuu ya polisi na kuzuia matangazo ya radio pamoja na mtandao wa simu katika mji mkuu wa Maseru.

Uchaguzi uliozongwa na utata nchini humo miaka miwili iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti.

Licha ya mazungumzo ya kuleta amani mnamo mwezi Juni ,hali ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo wakionya dhidi ya mbinu yoyote isio ya kikatiba.

Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana jirani yake kwa masli asli pamoja na nafasi za kazi.