Uchina yapinga uchaguzi huru Hong Kong

Haki miliki ya picha
Image caption Wanaharakati wa Demokrasi Hong Kong

Uchina imepinga uteuzi wa wazi wa kiongozi wa mji wa Hong Kong ifikiapo mwaka 2017.

Kamati ya baraza la kitaifa nchini humo imetangaza kwamba wagombea wote wanaowania wadhfa huo ni sharti waungwe mkono na kile ilichokitaja kuwa kamati ya uwakalishi mkubwa.

Wanaharakati wa demokrasi katika mji wa Hong Kong ambao ulikabidhiwa Uchina na taifa la Uingereza mwaka wa 1997 wanajianda kufanya maandamano dhidi ya uamuzi huo wa Beijing.

Awali katika eneo jirani la Macau jopo la Beijing linaloungwa mkono na serikali ya Uchina lilimchagua kwa mara ya pili Fernando Chui kuhudumu kwa miaka mitano kama kiongozi wa eneo hilo.