Thomas Tabane ahofia mapinduzi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Tabane

Msemaji wa waziri mkuu wa Lesotho,Thomas Thabane,amesema kua waziri mkuu huyo atakutana na raisi wa Africa Kusini,Jackob Zuma mjini Pretoria.Thabane alielekea nchini humo mwishoni mwa wiki,kwa mazungumzo huku akilishutumu jeshi kwa jaribio la kutaka kumng'oa madarakani.

Africa kusini imetoa kauli kua jaribio lolote la kuipindua nchi hiyo na kuvunja katiba halitavumilika.Naye mshauri wa karibu wa waziri huyo kua anataka kupinduliwa si kweli,na waziri huyo anatarajiwa kurejea nchini mwake ndani ya siku mbili zijazo.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanadai kua, kumekua na majaribio ya kutaka kuipindua serikali tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake mwaka 1966 na pia inakailiwa na machafuko ya kisiasa miezi ya karibuni.