Korea Kaskazini yawashikilia wamarekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mmoja wa wanaoshikiliwa

Raia watatu wenye asili ya Marekani,ambao wanashikiliwa Korea Kaskazini,wamezungumza na waandishi habari katika hali isiyokuwa ya kawaida,mahojiano yaliyoandaliwa na Pyongyang.

Raia hao ni Kennth Bae,Jeffrey Fowle na Matthew Miller wameomba watumwe viongozi wa juu wa serikali ya Marekani ili wakajadiliane kuhusu kuachiliwa kwao.

Wataalamu wa mambo wameyazungumzia mahojiano hayo kuwa Korea Kaskazini inachohitaji ni kuyamaliza mambo na si vinginevyo.

Kati ya hao wanaoshikiliwa mmoja wao Bae , hali yake si nzuri na anahitaji matibabu ya haraka, ambaye anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela kwa jaribio la kwenda kinyume na sheria za Korea Kaskazini.

Nao Miller na Fowle wao wanasubiri hukumu yao kwa kile Korea Kaskazini walichokiita kuleta uhasama.

Serikali ya Marekani nayo ikajibu ya kwamba mateka hao waachiliwe mara moja chini ya haki za binaadamu.