Wazazi wa Sotloff watoa kauli yao

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Steven Sotlof

Familia ya mwandishi wa habari Steven Sotloff hatimaye imezungumza kwa mara ya kwanza tangu mtoto wao auawe na wapiganaji wa dola ya Kiislam IS na picha za mauaji hayo kuonyeshwa.

Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo, Barak Barfi kutoka taasisi ya America Foundation think tank akiwa nyumbani kwao Pinecrest, Florida amemuelezea Sotloff kuwa ni mtu aliyefanya kazi yake kwa niaba ya wanyonge wa Mashariki ya kati.

Wanafamilia hao wamesema mtoto wao hakuwa tu shujaa bali ni wa namna yake ambaye daima alikuwa akitafuta kurejesha nuru palipo na giza.

Hata hivyo wazazi hao wa Steven walitoa heshima zao pia kwa kifo cha James Foley aliyechinjwa pia na wapiganaji hao wa dola ya Kiislam ya IS.