Mchekeshaji Joan Rivers aaga dunia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Enzi za uhai wake Joan Rivers

Mchekeshaji maarufu nchini Marekani Joan Rivers amefariki dunia akiwa na umri wa miaka themanini na moja.

Joan alikua amelazwa katika hospitali moja mjini New York kwa wiki kadhaa sasa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo.

Melissa binti wa Joan,akitangaza juu ya kifo cha mamake alimuelezea mama yake kua maishani mwake alikua akipenda kuona watu wana tabasamu usoni ama vicheko.

Joan River alianza shughuli zake za ucheshi kama muigizaji wa kawaida tu nusu karne iliyopita, na anatajwa kua mwanamke maarufu na bora katika ucheshi jukwaani.

Joan anayesifika sana kwa vichekesho vyake aliacha kupumua wakati alipofanyiwa upasuaji kooni katika kilini moja Alhamisi iliyopita.

"Mamangu alipenda sana kuchekesha watu na wakati wote alitaka watu wawe tu na furaha,'' alisema Rivers

Image caption Joan aliishi kujicheklea mwenyewe kutokana na upasuaji wa kujiongeza urembo ambao ulimuendea mrama

''Ingawa kipindi hiki ni kigumu kwangu, najua mamangu angependa sote tuanze kufurahia na kurejea katika hali zetu za kawaida,'' aliongeza kusema Melisa.

Muigizaji huyo alijulikana kwa kuwkosoa watu hasa waliovalia vibaya na hiovi karibuni alijulikana zaidi kwa kipindi chake cha Fashion Police katikakituo cha televisheni cha E.

Joana na mwanawe Melissa walihi kushiriki kipindi cha televisheni kilichojulikana kama 'Joan & Melissa: Joan Knows Best'

Waliomfahamu sana Joan ni wapenzi na waraibu wa mitindo ya mavazi ambao walikuwa wanafuatlia sana kipindi chake cha Fashion Police ingawa pia alijulikana kwa uigizaji na uchekeshaji.

Joan alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kuongeza mwili wake urembo kuanzia kwa pua lek, mdomo , uso wake na sehemu zengine za mwili wake. Baadhi ya upausuaji huo haukutokea vizuri na uso wake ulionekana kuwa na alama za upasuaji hu, na hicho kilikuwa kichekesho kwa Joan mwenyewe maana kila alipokuwa anawakejeli wenzake na yeye mwenyewe hajisaza maana alijichekelea.