Gremio yafungiwa ubaguzi michezoni

Image caption Gremio

Klabu maarufu ya soka nchini Brazili Gremio imefungiwa kushiriki mashindano makubwa kutokana na tuhuma za ubaguzi wa rangi michezoni.

Hatua hiyo imekuja kufuatia vitendo vya ubaguzi wa rangi wiki iliyopita wakati klabu hiyo ikicheza na Santos pale mashabiki wa Gremio walipomzomea na kupiga kelele za mfano wa nyani wakiashiria kumkataa golikipa huyo.

Hii si mara ya kwanza wachezaji wenye asili ya weusi kutengwa na kubaguliwa michezoni.