Ebola:Serikali kuwatenga raia Sierra L.

Haki miliki ya picha
Image caption Mwathiriwa wa ugonjwa wa Ebola abebwa na maafisa wa afya

Mshauri wa rais wa Sierra Leone ,moja ya taifa la afrika magharibi ambalo limeathiriwa vibaya na ugonjwa wa Ebola amesema kuwa serikali itaanzisha mpango wa siku nne wa kuwatenga raia ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Mpango huo utaanza tarehe 18 mwezi Septemba.Mshauri huyo Ibrahim Ben Kargabo amesema kuwa hatua hiyo itawawezesha maafisa wa afya kuwatafuta wagonjwa wa Ebola,na kuelezea kuwa ni njia mojawapo kusitisha ueneaji wa ugonjwa huo nchini Sierra Leone kabisa.

Amesema kuwa zaidi ya watu elfu ishirini watapelekwa katika makaazi ili kuhakikisha kuwa raia wanasalia majumbani mwao.

Tayari baadhi ya miji karibu na mpaka wa Guinea imetengwa.