Ebola:MSF yapinga mpango wa Sierra L

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mabango ya kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra leone

Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF limeonyesha wasiwasi wake kuhusu mpango wa siku tatu wa kuwatenga raia nchini Sierra leone ili kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.

MSF linasema kwamba katika uzoefu wake, kuwatenga raia kutasababisha watu wengi kuficha visa vipya vya ugonjwa huo swala litakalosababisha kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo.

Wafanyibiashara nchini Sierra leone pia wameukosoa mpango huo wakisema kuwa utaathiri mapato yao kwa siku tatu .

Zaidi ya watu elfu ishirini watapelekwa mashinani ili kutekeleza amri hiyo ya kutotoka nje inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi huu.