Ajitoa mhanga na kuwaua 12 Somalia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shambulizi hilo limetokea siku chache tu baada ya kiongozi wa Al Shabaab Ahmed Godane kuuawa

Taarifa kutoka mjini Mogadishu nchini Somalia, mlipuaji wa kujitoa mhanga amejilipua na kuwaua watu 12 katika msafara wa majeshi ya Muungano wa Afrika.

Mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga aligongesha gari alilokuwa anaendesha likiwa na mabomu kwenye msafara huo karibu na mji wa Afgoye Kaskazini Mashariki ya mji mkuu Mogadishu.

Wengi waliouawa walikuwa raia waliokuwa wanasafiri kwenye basi la abiria.

Zaidi ya watu 20 wameripotiwa kujeruhiwa. Mji huo umekuwa kitovu cha mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab.

Shambulizi hili limetokea siku chache baada ya Marekani kuthibitisha kumuua kiongozi wa Al Shabaab Ahmed Gofane.

Kadhalika kundi hilo lilikuwa limesema kuwa litalipiza kisasi mauaji ya kiongozi wake ila halikusema eneo ambalo watashambulia.