Human Right Watch waishutumu Israel

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahamiaji haramu nchini Israel

Shirika la Human Right Watch limesema Israel imewalazimisha takriban raia 7000 wa Eritrea na Sudan kuondoka nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika hilo la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch, raia hao walinyimwa njia za kuweza kupatiwa hifadhi, na kwamba jambo hilo ni kinyume cha sheria.

Mapema mwaka huum Wa Afrika waliokuwa wakiomba hifadhi nchini Israel waliandamana kupinga jinsi wanavyoshughulikiwa.

Hata hivyo kwa upande wake Israel imesema sera ya nchi hiyo, kuhusiana na wahamiaji haramu na wakimbizi inatekeleza sheria za kimataifa.

Inasisistiza kuwa Waafrika sio waomba hifadhi lakini ni wahamiaji kutokana na sababu za kiuchumi ambao wanaiona Israel kama kivutio kukidhi mahitaji yao kutokana na kuwa nchi iliyo karibu yao ambayo inamaendeleo, ambako wanaweza kupata kazi.