Agutuka na kuanza kuongea kichina

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Daktari anasema ni vigumu kueleza kichotokesa katika ubongo wa McMahon

Ben McMahon kutoka Melbourne, Australia, hawezi kukmbuka kuwa alikuwa hali mahututi alipohusika na ajali ya barabarani zaidi ya wiki moja iliyopita, lakini alichokikumbuka alipoamuka kutoka katika hali yake kinastaajabisha.

McMahon aliamka kutoka katika usingizi mzito yaani , 'Coma,' akiwa na uwezo wa kuzungumza kichina.

Wazazi wake walikuwa na furaha isiyo na kifani kupata taarifa za mwanao kuwa bukheri wa afya, lakini walipigwa na mshangao kugundua uwezo wake kwa kuzungumza lugha mpya.

McMahon alijifunza lahaja ya Mandarin akiwa shuleni , lakini ana kiri kuwa hakuwa na uwezo wa kuongea kichina.

Kwa siku zake za kwanza baada ya kutoka katika hali yake mahututi, McMahon angeweza tu kuzungumza na kuandika Mandarin. Ilimchukua muda kuanza kuweza kuongea kiingereza ambayo ndiyo lugha yake ya kwanza.

Hata baada ya kuanza kuzungumza kiingereza tena, uwezo wake wa kuongea Mandarin ulisalia.

Hii leo McMahon anatumia uwezo wake mpya wa kuongea lugha hiyo kwani anaishi na kusomea Shanghai, na pia ametumia muda wake kuwaelekeza watalii kutoka China na hata kuwa na kipindi cha kichina kwenye televisheni.

Daktari aliyemtibu McMahon amestaajabishwa na uwezo wake kuongea kichina na hata kuelezea kilichojitokeza katika mgonjwa wake kama jambo la kipekee ambalo limezua mjadala tayari.

Hata hivyo anasema kuwa sehemu ya ubongo wa McMahon iliyomsaidia kuongea kiingereza iliharibiwa katika ajali na kufanya sehemu ya akili yake iliyokuwa na ufahamu mdogo kuhusu kichina kuanza kutumika.

Vyovyote madakatri wanavyoka kuieleza hali hiyo,McMahon ana furaha ya kuendelea kuzungumza lugha mbili tofauti kwa sasa.