Sudan kusini na tishio la njaa

Haki miliki ya picha CAREJosh Estey
Image caption Mvua zinakwamisha usambazaji wa misaada S.kusini

Kufuatia zaidi ya miezi minane ya mapigano Sudan Kusini, sasa inakabiliwa na tishio la njaa.

Umoja wa Mataifa unasema takriban watu milioni nne wako katika hatari kubwa ya kukosa chakula baada ya wakulima kukosa kupanda msimu huu.

Mvua inayonyesha pia imeharibu barabara na kufanya juhudi za kutoa misaada kuwa ngumu zaidi.

Wataalam wameonya kuwa baa la njaa huenda likaikumba Sudan Kusini kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Mamilioni ya watu tayari wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.