Baba aua watoto watano-Marekani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Timothy baba wa watoto watano,aliowatoa uhai.

Mwanamume mmoja raia wa Marekani anashukiwa kuwaua watoto wake watano na kuwatupa katika jimbo jingine, hii ni kwa muujibu wa polisi nchini humo.

Timothy Ray Jones anakabiliwa na mashtaka kadhaa katika jimbo ambalo ndio makazi yake la Carolina ya kusini,kufuatia shutuma hizo na alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita huko Mississippi .

Watoto hao watano waliopoteza uhai kwa kuuawa na baba yao walikua na umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi miaka nane inaelezwa watoto hao watano walipotea katika mazingira ya kutatanisha , mama wa watoto hao aliporipoti polisi baada ya mawasiliano kati yake na mzazi mwenziwe kukatika.

Maafisa hao wa polisi walipofanya uchunguzi wao waligundua miili ya watoto hao imezikwa karibu na mji wa Alabama karibu na barabara kuu baada ya kuwasaka watoto hao kwa siku nzima .

Jones alisimamishwa katika kizuizi cha barabarani na kushukiwa kua alikua akiendesha gari baada ya kutumia dawa za kulevya ,imethibitika kuwa katika gari yake kulikuwa na kemikali zinazoaminika kua dawa za kulevya, zaidi ya hapo polisi walikuta damu garini mwake na alikua akitafutwa huko Carolina ya kusini .

Kitengo kinachoshulikia usalama wa raia huko Alabama kimesema kupitia kwa msemaji wake sajenti Steve Jarrett kwamba baada ya msako huo Jones baba wa watoto hao aliwaongoza maafisa hao hadi eneo alikozika miili ya wanawe.