Ebola yatishia usalama Liberia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mhudumu wa Afya akiwa amejikinga dhidi ya maambukizi ya ebola

Kusambaa kwa virusi vya ebola nchini Liberia, ni kitisho kikubwa kwa usalama wa nchi hiyo. Hiyo ni taswira iliyoelezwa na Waziri wa Ulinzi wa Liberia katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ugonjwa wa Ebola umeua watu zaidi ya elfu moja na mia mbili nchini Liberia. Rudolf von Ballmoos, ni balozi wa Liberia nchini Uingereza. Alipotembelea studio za BBC jijini London aliulizwa na mtangazaji wa Focus on Africa, Akwasi Sarpong, janga la ugonjwa wa ebola nchini Liberia limeonyesha kushindwa kwa uongozi wa nchi hiyo. Balozi Rudolf von Ballmoos amesema Serikali ya Liberia inafanya kila linalowezekana na kukiri kuwa kuna changamoto ya mfumo wa afya nchini Liberia ambao umekua tishio kwenye ukanda mzima.