Mahakama yazuia marufuku ya pombe India

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jimbo la Kerala ndilo lenye walevi wengi India

Mahakama ya rufaa nchini India imezuia mpango wa jimbo la Kerala Kusini mwa nchi hiyo kupiga marufuku pombe.

Mamia ya wamiliki wa baa walikuwa wamepinga marufuku hiyo ambayo ingeanza kutekelezwa Ijumaa hii kwa kusema kuwa itaporomosha utalii.

Hoteli za kifahari zingeponea marufuku hiyo na mahakama iliamua kuwa marufuku hiyo haina msingi.

Jimbo la Kerala ndilo lenye kiwango kikubwa zaidi cha walevi nchini India.

Uamuzi wa mwisho kuhusu swala hilo, utatolewa na mahakama kuu.