Muingereza aliyepona Ebola kurejea Afrika

Image caption Pololey amesema ana hamu sana kurejea Afrika kuwasaidia wagonjwa wengine

Mwanaume wa kwanza muingereza kuambukizwa homa kali ya Ebola, katika mlipuko wa ugonjwa huo unaoshuhudiwa katika kanda ya Afrika Magharibi, anatarajiwa kurejea Afrika ambako aliambukizwa.

Anasema anafanya hivyo ili aweze kuwasaidia wengine walioathirika kuweza kupambana na ugonjwa huo ambao ni janga kubwa

William Pooley alipokea matibabu mjini London baada ya kupelekwa nchini humo kutoka Sierra Leone.

Ameweza kupona na hata kuodnoka hospitalini. Lakini kwa sasa anajiandaa kusafiri kurejea Afrika katika wiki chache zijazo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wamekuwa wakihamasishwa kujizuia na maambukizi kwa kuweka usafi

Pooley mwenye umri wa miaka 29, alisema ana hamu kubwa sana kurejea Afrika na kwamba huenda asiweze kuambikizwa.

Wakati Pooley alipoambukizwa, alikuwa anafanya kazi ya kujitolea nchini Sierra Leone, ambayo ni moja ya nchi za kanda ya Afrika Magharibi zilizoathriwa na ugonjwa huo.

Takribna nusu ya watu 3,000 waliombaukizwa homa hiyo, katika mlipuko wa sasa barani Afrika, ambao ilianzia nchini Guinea, wamefariki.

''Nina hamu sana kurejea kufanya kazi inayonisubiri,'' Pooley aliambia BBC.

"nahisi kama zijaimaliza kazi yangu kwani niliondoka huko mapema sana. Na ninajua kuna kazi nyingi katika nchi hizo, na tunahitaji kuwa huko kuwasaidia watu. ''