Waliomshambulia Malala wakamatwa

Image caption Malala ni mwanaharakati anaysifika sana duniani kwa kutetea wasichana wapate elimu

Jeshi nchini Pakistan linasema limewakamata watu 10 wanaoshukiwa kupanga na kufanya shambulio dhidi ya msichana wa shule nchini humo Malala Yusufzai.

Msemaji wa jeshi meja jenerali Asim Salim Bajwa amesema silaha iliotumika katika shambulio hilo imepatikana.

Amesema kundi hilo liliagizwa na mkuu wa kundi la Taliban, Mullah Fazlullah, kutekeleza shambulio hilo.

Malala Yousufzai alipigwa risasi mara tatu kwa karibu miaka miwili iliyopita na wanaume waliojihami kwa bunduki walipanda basi la shule alimokuwa Malala, katika wilaya ya Swat iliyopo kaskazini magharibi mwa Pakistan na wakamuita kwa jina.