Benki zapinga kujitenga kwa Scotland

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Benki ya Scotland

Huku ikiwa imesalia siku chache tu kabla ya raia wa Scotland kushiriki katika kura ya maamuzi kuhusu uhuru wa Scotland kutoka kwa Uingereza,kumekuwa na majibizano makali kuhusu jukumu linalochukuliwa na wafanyibiashara.

Naibu kiongozi wa zamani wa chama kinachopigania uhuru wa Scotland Jim Sillars, amezionya benki kwamba zitakabiliwa na wakati mgumu iwapo matokeo ya kura hiyo ya maamuzi itaunga mkono kujitenga.

Taasisi kadhaa za kifedha awali zilithibitisha kuwa zitahamisha afisi zao hadi mjini London iwapo kura hiyo itaunga mkono uhuru wa Scotland .

Kura za maoni zinasema kuwa matokeo ya kura hiyo huenda yakaenda upande wowote.