Wanachama 100 wa Boko Haram wauawa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption jeshi la Nigeria

Jeshi la Nigeria linasema kuwa limewaua zaidi ya wanamgambo 100 wa kundi la Boko Haram kufuatia shambulizi la wapiganaji hao siku ya ijumaa kazkazini mashariki mwa jimbo la Borno.

Vikosi vya serikali vimeripotiwa kuyakamata magari na risasi wakati vilipokuwa vikiimarisha usalama katika mji wa Konduga,yapata kilomita 35 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo, Maiduguri.

Wapiganaji wa Boko Haram wameiteka miji kadhaa na vijiji katika majuma ya hivi karibuni wakikaribia kuelekea Maiduguri.