Mamia ya wahamiaji wafa maji

Image caption boti

Mamia ya wahamiaji wamekufa maji wakati wakijaribu kuelekea nchini Italia kupitia Bahari ya Meditarian ambapo boti yao ilizama karibu na kisiwa cha Malta wakati wakijaribu kuelekea nchini Italia.

Manusura wawili raia wa Palestinian wamelieleza shirika la kimataifa la uhamiaji la IOM jinsi ajali hiyo ilivyotokea na kwamba ilisababishwa na vurugu kati ya abiria hao na wafanya biashara za magendo..

Msemaji wa shirika la IOM Leonard Doyle ameiambia BBC kuwa watu wawili walionusurika katika ajali hiyo wamesema mazingira ya kuzama kwa boti yao ilitokea pale walipolazimishwa kuhamia katika chombo kingine na walipokataa vurugu ikaanza.

Doyle anasema kuwa watu hao wamesema kuwa walianza safari hiyo katika bandari ya Damietta nchini Misri Septemba wakiwa 500.

Shirika la umoja wa mataifa linasema wahamiaji wapatao 130,000 wamefanikiwa kuingia Ulaya kupitia bahari ya Mediteranian ambapo kwa mwaka huu pekee wahamiaji 80,000 wamepitia njia hiyo.

Kwa mjibu wa ripoti ya umoja wa mataifa Italia imepokea wahamiaji 118,000.