NASA yashindwa kubaini vimondo

Haki miliki ya picha NASA
Image caption shughuli zikiendelea anga za juu

Shirika la safari za anga la juu nchini Marekani NASA,imeoneshwa ukinzani kutokana na kushindwa kung'amua vitu vya hatari angani.

Shirika hilo linajaribu kubainisha vimondo na vitu vingine ambavyo hupita katika umbali wa kilomita milioni arobaini na tano katika uso wa dunia ili kujaribu kuilinda kutokana na hatari inayoweza kutokea.

Lakini mpaka sasa NASA imegundua asilimia kumi ya makisio yake na haidhaniwi kua malengo iliyojiwekea mpaka kufikia mwaka 2020 endapo yatafikiwa na huku muda wa mwisho wa kutoa ripoti kuhusiana na masuala ya anga ukifikia tamati.

Vimondo na vitu vingine husambaratishwa angani kabla havijaufikia uso wa dunia lakini vingine si rahisi.mwaka wa jana kimondo kimoja kiliripuka huko Urusi katika mji wa Chelyabinsk kikiwa na kasi kuwa wakati kikishuka mjini humo kasi ambayo ni mara thelathini zaidi ya bomu la atomic lililotupwa Hiroshima.