Walinda amani wasambazwa-Syria

Haki miliki ya picha epa
Image caption vikosi vya umoja wa mataifa

Umoja wa mataifa umesambaza maelfu ya walinda amani huko Syria katika eneo la Golan ambalo linamilikiwa na Israel.

Hatua hiyo inafuatia wiki mbili baada ya wapiganaji walioko mstari wa mbele huko Nusra,ambao ni waasi wa Syria kutoka kundi la Al-Qaeda, ambao tayari wameshateka walinda amani wapatao arobaini wa umoja wa mataifa na inaarifiwa kuwa walinda amani hao wamekwisha achiliwa huru.

Mwanaharakati wa upinzani nchini Syria ameeleza kuwa kikosi cha waasi kinashikilia eneo lote la Golani nchini Syria.