Jaji Masipa atishiwa baada ya uamuzi

Haki miliki ya picha
Image caption Jaji ni Masipa ni mwanamke wa pili mwafrika kushikilia wadhifa wake

Mashirika ya kisheria nchini Afrika Kusini, yameelezea wasiwasi kuhusu vitisho dhidi ya jaji aliyetoa uamuzi katika kesi inayomkabili mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius.

Jaji Thokozile Masipa alimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia wala sio mauaji ya kusudi.

Jaji huyo amekuwa akikosolewa tangu kutoa uamuzi wake kuwa Pistorius alimuua mpenzi wake kwa bahati mbaya.

Baadhi ya matamshi yaliyotolewa ni ya chuki , kumlimbikizia lawama na hata kwenda kinyume na mahakama.

Bi Masipa amewekewa ulinzi tangu kutoa uamuzi wake, kwa mujibu wa jarida la City Press.

Maafisa wa polisi wamekuwa wakishika doria nje ya nyumba yake na pia wamekuwa wakimsindikiza kila anapokwenda.

Pistorius alikana kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kukusudia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jaji ni Masipa anatarajiwa kutoa uamuzi dhidi ya Pistorius baada ya kumpata bila kosa la kukusudia kuua

Wataalamu wa maswala ya kisheria wamekosoa uamuzi wa jaji Masipa ambaye alichukua wadhifa wake mwaka 1998 na kuwa mwanamke wa pili mweusi kuwahi kushikilia wadhifa huo.

Taarifa ya wanasheria hao ilisema kuwa uamuzi wa jaji Masipa ilikuwa sawa kuambatana na sheria na pia kulingana na ushahidi uliotolewa Masipa.

Viongozi wa mashitaka walilaani uamuzi wa jaji Masipa wakisema kuwa Pistorius alipaswa kupataikana na hatia ya kumuua mpenzi wake kwa kukusudia.