Westgate:mwaka1 baadaye tumejifunza nini ?
Huwezi kusikiliza tena

Westgate:Mwathiriwa asimulia yaliomsibu

Ukiwa unakaribia mwaka mmoja sasa tangu lifanyike shambulizi la kigaidi katika maduka ya Westgate mjini Nairobi ambapo watu sabini waliuawa na wengine kujeruhiwa, idhaa ya BBC inaangazia makala maalum kuhusu kilichobadilika tangu mashambulizi hayo kufanyika, hasa katika nyanja za usalama.

Kuanzia leo Idhaa ya Kiswahili ya BBC itakuletea mfululizo wa makala maalum kuelekea siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya tukio hilo siku ya Jumapili.

Dennis Okari amezungumza na mmoja wa walionusurika Anne Moraa ambaye alikuwa akifanya kazi ya kusimamia mauzo katika duka moja wapo ndani ya jengo hilo la Westgate.