Ebola kuharibu uchumi wa Liberia

Banki ya dunia imetoa tahadhari kuwa mlipuko wa ugonjwa wa ebola huenda ikaleta balaa ya kiuchumi katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Benki hiyo imeeleza kuwa athari ya kiuchumi kutokana na virusi hivyo itaongezeka mara nane zaidi kwa nchi hizo ambazo uchumi tayari umeshaporomoka, Liberia ndio inayoonekana kuathirika zaidi ambapo uchumi wake utashuka kwa asilimia kumi na mbili ya kipato cha nchi hiyo.

Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema limependekeza mikopo kwa jumla ya dola milioni mia moja na ishirini na saba kwa nchi tatu zilizoathirika na ugonjwa wa ebola, ili kuwasaidia kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo.