Ebola:Guinea yawasaka maafisa waliotekwa

Mmoja wa wathiriwa wa ugonjwa wa Ebola Guinea aliyefariki
Maelezo ya picha,

Mmoja wa wathiriwa wa ugonjwa wa Ebola Guinea aliyefariki

Guinea imeanza kufanya msako kuwatafuta maafisa wa afya walioshambuliwa siku mbili zilizopita.

Maafisa hao walikuwa wamekwenda kijijini kuwahamasisha wanakijiji kuhusu Ebola

Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinasema kuwa huenda watu hao walitekwa nyara.

Maafisa hao walitoroka kijiji cha Wamey katika eneo la Nzerekore baada ya kurushiwa mawe.

Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola umewaa watu 2,622 nchini Guinea sawa na Liberia na Sierra Leone.

Mlipuko huu wa Ebola ndio mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani , huku maafisa wa afya wakionya kuwa huenda watu wengine zaidi ya 20,000 wakaathiriwa.

Mwezi jana vurugu zilizuka katika eneo ambako wafanyakazi hao walitoweka.

Eneo hilo linakaribiana na eneo ambalo lilikuwa la kwanza kukumbwa na ugonjwa huo kufuatia fununu kwamba wauguzi walikuwa wanawaambukiza watu ugonjwa huo walipokuwa wanapuliza dawa ya kuzuia maambukizi katika soko moja.

Watu waliotoweka wanaaminika kuwa waandishi wa habari pamoja na maafisa wengine wa afya.