Ufaransa yaishambulia Islamic State Iraq

Ufaransa imetekeleza mashambulizi ya kwanza dhidi ya Islamic State
Maelezo ya picha,

Ufaransa imetekeleza mashambulizi ya kwanza dhidi ya Islamic State

Ufaransa imetekeleza mashambulizi yake ya kwanza ya angani dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wa Islamic State nchini Iraq.

Rais wa Ufaransa ilisema kuwa ndege za Ufaransa zilishambulia ngome za IS kaskazini mashariki ikiongeza kuwa kutakuwa na mashambulizi zaidi siku zinazokuja.

Aidha iliongezea kusema kuwa handaki za Islamic State zililengwa katika mashambulizi hayo.

Ndege za Ufaransa ambazo ziko katika nchi ya miliki za kiarabu UAE zimekuwa zikifanya uchunguzi nchini Iraq tangu Jumatatu.

Siku ya Alhamisi rais wa Ufaransa Francois Hollande alithibitisha kuwa alikubaliana na ombi la Iraq la msaada wa jeshi la anga.

Islamic State inadhibiti eneo kubwa nchini Iraq na pia Syria ambapo ilikuwa imetangaza himaya yao.

Mashambulizi hayo yalifuatia msaada wa zana za kivita kwa wapiganaji wa kikurdi ambao wanatarajiwa kuzitumia kupambana na kundi la IS.

Maelezo ya picha,

Islamic State inadhibiti asilimia kubwa ya Ardhi nchini Iraq na Syria

Hata hivyo rais huyo alisema kuwa hakutakuwa na wanajeshi wa nchi kavu wa kifaransa watakaotumwa kupambana na IS Iraq.

Ndege hizo aina ya Rafale zilishambulia mji wa Zumar, kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Iraq

Qassim al-Moussawi.

Muungano huo unaojumuisha washirika wa Marekani pia unajumuisha ndege za uchunguzi za Uingereza na Australia.