Marekani:Iran ina jukumu dhidi ya IS

John Kerry
Maelezo ya picha,

John Kerry

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amesema kuwa Iran ina jukumu la kutekeleza katika juhudi za kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq na Syria.

Bwana Kerry ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba muungano wa kuliangamiza kundi hilo una majukumu mengine mbali na hatua za kijeshi na kwamba huenda Iran ikashirikishwa.

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani imebaini kwamba wawakilishi wa Iran na wale wa Marekani wamejadiliana kuhusu tishio linalosababishwa na wapiganaji hao kandokando ya vikao vya mkutano kuhusu mpango wa nuklia wa Iran.