Ahadi za kampeni zaibua tofauti Scotland

David Cameron
Maelezo ya picha,

David Cameron

Tofauti zimeibuka kati ya vyama vikubwa nchini Uingereza kuhusu mabadiliko walioahidiwa wapiga kura wa Uskochi kama hatua mbadala ya kujitenga.

Chama cha waziri mkuu nchini Uingereza cha Conservative kinasema kuwa mpango wa kuipa serikali ya Uskochi mamlaka zaidi ni lazima uambatane na mabadiliko kuhusu vile sera zinazoathiri Uingereza hukabiliwa katika bunge la Uingereza.

Hatahivyo chama cha Upinzani cha leba kinasema kuwa maswala hayo mawili ni sharti yakabiliwe tofauti ,ili kuhakikisha kuwa ahadi walizopewa wapiga kura wa Uskochi zinaafikiwa mara moja.

Taifa la uskochi lilikataa kujitenga na Uingereza katika kura ya maamuzi.