Afghanistan yabuni serikali ya umoja

John Kerry,Ashraf Ghani na Abdullah Abdulla
Maelezo ya picha,

John Kerry,Ashraf Ghani na Abdullah Abdulla

Makubaliano ya kubuni serikali ya umoja wa kitaifa nchini Afghanistan hatimaye yametiwa sahihi ,baada ya miezi kadhaa ya mgogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais mnamo mwezi April na Juni.

Katika makubaliano hayo ya kugawana mamlaka Ashraf Ghani ndio rais mpya huku mpinzani wake Abdullah Abdullah akimchagua afisa mkuu atakayekuwa na mamlaka kama yale ya waziri mkuu.

Ashraf Ghani atakuwa rais mpya mwenye mamlaka mengi na makubaliano hayo yanasema kuwa afisa mkuu atakayechaguliwa atakuwa akiwajibika kwake.

Hatahivyo bwana Ghani amepoteza harakati za kutaka kutawazwa baada ya matokeo ya uchaguzi.

Wawili hao wametia sahihi makubaliano ya kubuni serikali ya kitaifa kabla ya matokeo hayo ya uchaguzi kutangazwa.

Na afisa mkuu atakayechaguliwa na Abdulla Abdullla atakuwa sako kwa bako na rais wakati atakapotawazwa.

Bwana Abdullah alikabidhiwa uwezo wa kuwateua maafisa wengine wa ngazi za juu dhidi ya Ghani.

Makubaliano hayo yanasema kuwa makundi hayo mawili yatashirikishwa vilivyo katika uongozi wa taifa hilo.

Hatahivyo hakutakuwa na usawa wa kuwateua maafisa zaidi katika ngazi za chini za serikali swala ambalo huenda likazua ubishi mkubwa.

Lakini baada ya mgogoro mkubwa wa kampeni za uchaguzi wa miezi kadhaa,udhabiti wa taifa hilo haujulikani.