Boko Haram lashambulia Nigeria Kazkazini

Wapiganaji wa Boko Haram
Maelezo ya picha,

Wapiganaji wa Boko Haram

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wameshambulia mji wa kazkazini mashariki wa Mainok karibu na mji wa Maiduguri.

Takriban watu thelathini wameripotiwa kufariki siku ya ijumaa wakati wapiganaji hao walipotekeleza mashambulizi katika soko moja lililojaa watu wakati wa mchana.

Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji hao walibeba chakula katika magari ya wizi,huku wanajeshi wakitoroka.

Kundi la Boko haram limechukua udhibiti wa miji kadhaa na vijiji katika mji wa Maiduguri katika majuma ya hivi karibuni.

Jeshi limejaribu kulikabili kundi hilo licha ya tangazo la hali ya hatari katika majimbo mjatatu ya kazkazini mashariki mwa Nigeria mwaka uliopita.