watu 67 wauawa kenya

Wapiganaji wa Al Shabaab
Maelezo ya picha,

Wapiganaji wa Al Shabaab

Raia wa Sierra Leone wamesalia majumbani mwao kwa siku ya pili mfululizo wakati ambapo taifa hilo linatekeleza agizo la kutotoka nje la masaa 72 ili kujaribu kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.

Mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Freetown anasema kuwa barabara nyingi za miji ambazo zimekuwa zikijaa watu hazina watu kwa sasa.

Mwandishi huyo amesema kuwa kituo cha oparesheni za dharura kilipokea zaidi ya simu 900 katika siku ya kwanza ya agizo hilo,kupitia kuwaripoti wagonjwa ama kutaka miili ya wafu kuchukuliwa.

Amesema kuwa kuna vituo viwili pekee katika taifa hilo na kwamba kituo kimoja katika eneo la Kenema kimejaa wagonjwa.

Virusi vya ugonjwa huo vimeathiri nyumba na jamii nyingi nchini humo kwa kuwa zilishindwa kuripoti visa vya kwanza vya ugonjwa huo.

Vituo vya kuwatenga wagonjwa vimejengwa katika mji wa Freertown katika siku chache zilizopita ambapo watu wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa huo watapelekwa huku matokeo yao ya kubaini iwapo wanaugua ugonjwa huo yakisalia.

Maelfu ya maafisa wa polisi wamesambazwa ili kuwalinda maafisa wa afya.