Mlipuko wawaua watu wawili nchini Misri

Mlipuko nchini Misri
Maelezo ya picha,

Mlipuko nchini Misri

Kumekuwa na mlipuko karibu na jumba la wizara ya maswala ya kigeni nchini Misri.

Ripoti za awali zinasema kuwa watu wawili waliuawa katika mlipuko huo katika wilaya ya Bulaq Abu-al-lla, eneo lililojaa watu katika mto Nile.

Tangu kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi mnamo mwezi July mwaka jana ,misri imekuwa ikishuhudia misururu ya milipuko na mashambulizi yanayowalenga maafisa wa polisi na wanajeshi.