Ebola:Raia wa Sierra.L waheshimu agizo

Mitaa ya Siera Leone
Maelezo ya picha,

Mitaa ya Siera Leone

Raia wa Sierra Leone wamesalia majumbani mwao kwa siku ya pili mfululizo wakati ambapo taifa hilo linatekeleza agizo la kutotoka nje la masaa 72 ili kujaribu kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.

Mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Freetown anasema kuwa barabara nyingi za miji ambazo zimekuwa zikijaa watu hazina watu kwa sasa.

Mwandishi wetu anasema kuwa kituo cha oparesheni za dharura kilipokea zaidi ya simu 900 katika siku ya kwanza ya agizo hilo,kupitia kuwaripoti wagonjwa ama kutaka miili ya wafu kuchukuliwa.

Amesema kuwa kuna vituo viwili pekee katika taifa hilo na kwamba kituo kimoja katika eneo la Kenema kimejaa wagonjwa.