Wakenya waadhimisha tukio la kigaidi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maduka ya Westgate

Sherehe tofauti zinafanyika nchini Kenya ili kuadhimisha mwaka mmoja tangu shambulizi la kigaidi la maduka ya West Gate,ambapo takriban watu 67 walipoteza maisha yao ikiwemo washukiwa wanne wa shambulizi hilo.

Kanda ya video ya CCTV kuhusu shambulizi hilo inaonyesha wateja wa duka hilo walioshtuka wakiwatoroka majambazi hao huku wengine wakijificha chini ya meza za maduka yao.

Kundi la wapiganaji wa Alshabaab lilikiri kutekeleza shambulizi hilo.

Siku ya jumamosi ,mkuu wa polisi nchini Kenya alitoa wito kwa raia kuwa macho ili kuepuka shambulizi lolote la kigaidi linalolenga kuambatana na maadhamisho hayo.