Marufuku ya kutoka nje tamati S.Leone

Raia walilazimika kujifungia ndani kupambana na ebola
Maelezo ya picha,

Raia walilazimika kujifungia ndani kupambana na ebola

Serikali nchini Sierra Leone imesema kuwa mpango walioutangaza kwa raia kutotoka nje kwa siku tatu kwa ajili ya kupambana na maradhi ya Ebola umefanikiwa .

Amri hiyo iliyotekelezwa kwa siku tatu imemalizika usiku wa jumapili na kuwa muda hautaongezwa tena.

Sierra Leone ni moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na Ebola, Watu 550 wakiripotiwa kuathiriwa na ugonjwa huo na vifo vilivyoripotiwa 2,600

Wakati huo huo, nchi jirani Liberia imetangaza kuongezwa vitanda zaidi kwa ajili ya Wagonjwa wa Ebola.

Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani, WHO Hali ya ugonjwa huu ni mbaya afrika magharibi.Virusi vinaelezwa kusambazwa kwa njia ya jasho, damu na mate na hakuna tiba iliyothibitishwa.