Visa vipya 130 vya Ebola Sierra Leone

Kanda ya Afrika Magharibi ndiyo iliyoathirika zaidi kutokana na janga la Ebola
Maelezo ya picha,

Kanda ya Afrika Magharibi ndiyo iliyoathirika zaidi kutokana na janga la Ebola

Sierra Leone inasema kuwa imegundua visa vipya 130 vya maambukizi ya Ebola katika siku tatu ambapo serikali imeweka amri ya kutotoka nje ambayo ilikamilika Jumapili usiku.

Watu wengine 39 wangali wanafanyiwa uchunguzi kubaini ikiwa wameambukizwa ugonjwa huo.

Mkuu wa kitengo cha dharura cha kukabiliana na ugonjwa huo, (Stephen Gaojia), alisema kuwa amri ya kutotoka nje angalau imefanikisha juhudi dhidi ya ugonjwa huo.

Serikali ya nchi hiyo iliamrisha raia wake milioni sita kusalia majumbani kwa muda wa siku tatu katika juhudi za kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.

Ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu mbili na miasaba katika kanda ya Afrika Magharibi tangu mwezi Machi.