Dunia itunze mazingira :Ban Ki Moon

Ban ki Moon
Maelezo ya picha,

Ban ki Moon

Mataifa yenye mchango mkubwa katika uharibifu wa mazingira duniani yanaendelea na mkutano unaofanyika umoja wa mataifa Newyork Marekani ili kutafuta suluhu ya pamoja ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Zaidi ya nchi 120 viongozi wake wanahudhuria mkutano huo huku nchi mbili kinara katika kuchangia uharibifu wa mazingira duniani ambazo ni China na India viongozi wake hawatahudhuria.

Siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano huo katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa suala la mabadiliko ya tabia nchi lina umhimu wake kwa sasa na hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa.

Mwisho wa mkutano huo umoja wa mataifa nan chi washirika kuunda mikataba mipa ya kimataifa inayolenga kupunguza kasi ya mabadiliko tabia nchi.