Is wanamshikilia mateka mwingine

John Cantlie
Maelezo ya picha,

John Cantlie

Wanamgambo wa islamic state wametoa video nyingine inayomuonyesha mwandishi wa uingereza John Cantlie aliyekuwa ametekwa nyara.

Cantlie akiongea katika video hiyo ya dakika sita amesema alikuwa ametelekezwa na serikali yake na kwamba nchi za Magharibi zilikuwa zimepuuza uwezo wa wanamgambo wa IS.

Cantlie alitekwa huko syria mwaka 2012 ,na video yake inafanana na ile iliyotolewa wiki chache zilizopita ambapo alisema alikuwa ni mmoja wa wafungwa katika kundi.

IS tayari imeua mateka watatu wa nchi za magharibi na wamenuia kuua waingereza wanaofanya kazi ya kutoa misaada wanaowashikilia mateka.